Upo uwezekano mkubwa wa kumbi nyingi za starehe Bongo kufungiwa kutokana na tamko lililotolewa na serikali hivi karibuni kuwa, kumbi zote ambazo hazijasajiliwa hazitakiwi kuendelea kufanya kazi.
Akizungumza katika kikao kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Ghonche Materego alisema kuwa, zoezi zima la kuzihakiki kumbi hizo litafanywa na Kampuni ya Majembe ambao wamesaini nao mkataba.
“Tumeingia mkataba wa mwaka mmoja na Kampuni ya Majembe kuhakikisha kumbi zote za starehe zinasajiliwa, zile zitakazobainika kuendeshwa kiujanjaujanja hatua za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pomoja na kuzifungia,” alisema Materego.
Kufuatia mpango huo, imetabiriwa na baadhi ya wadau wa burudani nchini kuwa, kuna uwezekano kumbi nyingi zikafungiwa kufuatia uwepo wa nyingi ambazo hazijasajiliwa.
No comments:
Post a Comment