Zifuatazo ni njia sahihi zinazoweza kusaidia kumsafisha mtu aliyenaswa kwenye usaliti.
KWANZA: Ikiwa utajikuta upo kwenye dhambi ya usaliti ambayo huwezi kuikana njia ya kwanza kufanya ni kukiri kosa mbele ya mwenza wako na kumweleza mazingira yaliyosababisha wewe kufikia hatua ya kufanya usaliti.
“Nakiri mke wangu kuwa nimekosa kilichotokea kwenye hili ni kwamba huyu mwanamke nilikuwa naye tangu zamani na huwa haishi hapo lakini wiki hii alikuja jijini akanipigia simu nikakutana naye ndiyo hapo ibilisi alipoanza, lakini kusema kweli najuta kukukosea.” Huu ni mfano wa maneno ya kukiri kosa kwa kueleza sababu za usaliti wako.
PILI :Naamini kuna watu ambao hufanya usaliti kwa sababu ya dhaifu, hawa ni wale ambao tabia zao si za kujali heshima ya ndoa zao. Kwa hawa na wengine lazima hatua ya pili iwe ni kubadili mfumo wa maisha yao kwa ujumla.
Kwa mfano, ikiwa mtu amegundulika kuwa hufanya usaliti anapochelewa sana kurudi nyumbani au anapokuwa kwenye kumbi za starehe usiku, anachotakiwa kufanya ni kubadili mfumo mzima wa maisha yake ikiwa ni pamoja na kuacha kuchelewa na kwenda kwenye kumbi za usiku hapa ndipo atakapokuwa na nafasi ya kusamehewa na kuaminiwa.
TATU: Toba ya kweli yenye kuaminika lazima iambatane na matendo. Unapojikuta kwenye dhambi ya kusaliti lazima utubu kwa matendo yatakayoonyesha kweli unampenda mpenzi wako zaidi ya yule uliyekuwa naye. Hapa mambo ya zawadi, huduma na kujali lazima yachukue nafasi kubwa, lengo ni lile lile kujenga imani zaidi.
NNE: Kama kweli utakuwa umedhamiria kuomba radhi, basi lazima muonekano wako na maneno yako yatafsiri nia yako. Haiwezekani ukawa unamuomba radhi mtu huku ukitembea tembea na kuonyesha mzaha na hali ya uchangamfu kana kwamba ulichokifanya kilikuwa sahihi.
No comments:
Post a Comment