Nyaraka za siri za Marekani zipatazo 250,000 zimeanza kuwekwa hadharani pamoja na serikali ya Marekani kuionya tovuti ya WikiLeaks kuwa inavunja sheria na inayaweka maisha ya watu wengi hatarini. Tovuti ya WikiLeaks ambayo imebobea kwa kutoboa siri za ndani za masuala mbalimbali duniani ilikabiliwa na mashambulizi ya hackers ambao waliifanya tovuti hiyo ishindwe kupatikana online. Hata hivyo nyaraka hizo za siri zimewekwa hadharani kama ilivyopangwa kwa kutumia magazeti ya The Guardian la Uingereza, gazeti la New York Times la Marekani, Der Spiegel la Ujerumani, El Pais la Hispania na gazeti la Le Monde la Ufaransa. Nyaraka hizo za siri huenda zikaharibu uhusiano wa Marekani na baadhi ya viongozi wa nchi mbalimbali duniani ambao Marekani iliwapachika majina mbalimbali ya kuwakashifu. Miongoni mwa nyaraka hizo za siri hizo ni mazungumzo ya siri kati ya Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia ambaye mara nyingi sana alikuwa akiishinikiza Marekani ipigane vita na Iran ili kuziteketeza silaha zake za nyuklia. Taarifa hizo ziliendelea kusema kuwa Mfalme huyo wa Saudia aliishinikiza Marekani iiwekee Iran vikwazo vikali vya kiuchumi na kuwapiga marufuku viongozi wake kusafiri kimataifa. Nyaraka hizo ziliendelea kusema kuwa Mfalme Abdullah aliungwa mkono na Mfalme wa Bahrain, Hamad ibn Isa Al Khalifa na Mtawala wa Abu Dhabi, Sheikh Mohammad bin Zayed ambao nao waliitaka Marekani iiteketeze Iran. WikiLeaks pia ilitoa nyaraka ambazo zilisema kuwa Marekani kwa kuwatumia maafisa wake kinyume cha sheria iliwapeleleza viongozi wa baraza la Umoja wa Mataifa na hata kufikia kuchukua kwa siri alama za mboni ya jicho na alama za vidole za katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon. Marekani pia ilifuatilia simu walizokuwa wakipiga, fax, email na tovuti walizokuwa wakizitembelea. Miongoni mwa majina ya kashfa waliyopachikwa viongozi wa serikali mbalimbali duniani, Marekani ilimuita Rais Mugabe wa Zimbabwe kuwa ni "Kichaa Mzee", kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi ameitwa "Mtu wa Ajabu Asiyeeleweka", wakati rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad amefananishwa na Hitler. Nyaraka nyinginezo zilielezea jinsi Marekani ilivyokuwa ikizishinikiza baadhi ya nchi ziwachukue wafungwa wa kigaidi wa jela ya Guantanamo Bay. Nchi ya Slovenia ililazimishwa imchukue mfungwa mmoja wa Guantanamo Bay iwapo inataka kukutana na Rais Obama. Nyaraka zaidi za siri zinazoonyesha jinsi Marekani ilivyokuwa ikivunja sheria za kimataifa zinaendelea kuchapishwa. | ||
Siri za Marekani Zaanikwa Hadharani
Kitabu cha Mafunzo ya Wizi
Mwizi wa nchini Japan, Hajime Karasuyama kutokana na utaalamu wake wa kuiba kwenye majumba ya watu, ametoa kitabu kinachoelezea jinsi ya kuiba kwa ustadi mkubwa bila ya kugundulika. Kitabu chake kinachoenda kwa jina la "Kazi: Mwizi, Kipato Kwa mwaka: Yen Milioni 30", kimekuwa gumzo nchini Japan na kimekuwa kikinunuliwa kama njugu. Wachapishaji wa kitabu hicho Futabasha Publishing wamesema kuwa nakala za mwanzo za kitabu hicho zipatazo 10,000 zimenunuliwa zote ndani ya siku 10 baada ya kitabu hicho kuzinduliwa. Katika kitabu hicho, Karasuyama anaelezea jinsi ya kufungua vitasa vya milango ya aina yoyote ile kwa muda mfupi na bila ya ufunguo na jinsi ya kuvunja madirisha ya vioo bila ya kusababisha kelele. Karasuyama ameelezea pia jinsi alivyokuwa akitumia lensi kuangalia ndani ya nyumba kwa kupitia kwenye tundu la funguo. Mbali ya wizi wa majumbani, Karasuyama pia amelezea pia njia za kufanya utapeli na kuwaacha watu kwenye mataa. Karasuyama alisema kuwa kutokana na wizi alikuwa akijiingizia kitita kinono kwa mwaka zaidi ya Tsh. Milioni 540. "Tunapoingia ndani ya nyumba, sisi wezi huwa tunajua wapi watu huficha pesa zao", alisema Karasuyama alipokuwa akiongea na jarida la Shukan Taishu kuhusiana na kitabu chake ambacho kimeambatanisha maneno ya "Usijaribu kuniiga" kwenye ukurasa wake wa kwanza. Wachapishaji wa kitabu hicho kinachouzwa Yen 1,200 sawa na Tsh. 20,000 wamekanusha madai kuwa kuchapishwa kwa kitabu hicho kutapelekea baadhi ya watu kugeuka wezi kwa kuiga staili za wizi za Karasuyama. Wachapishaji hao wamesema kuwa kitabu cha Karasuyama kitawawezesha watu kujifunza njia zinazotumiwa na wezi hivyo kuweza kuzilinda vyema nyumba zao. | ||
Mnigeria Awa Mbunge Wa Kwanza Mweusi Nchini Poland
John Abraham Godson, alizaliwa katika jimbo la Abia nchini Nigeria na alikulia nchini humo kabla ya kuhamia nchini Poland. Godsnon ambaye ni msomi mwenye shahada nyingi, amekuwa gumzo nchini Poland baada ya kuingia kwenye vitabu vya historia ya masuala ya siasa nchini humo kwakuwa mtu mweusi wa kwanza kuwa mtunga sheria wa bunge la nchi hiyo ambayo bado ina matatizo ya ubaguzi wa rangi. Godson alishawahi kuonja joto la ubaguzi wa rangi nchini humo kwa kushushiwa kipigo mara mbili bila ya sababu za msingi. Godson alihamia Poland mwanzoni mwa miaka ya 1990 na kuanzisha shule ya Kiingereza na pia kufanya kazi kama mchungaji wa kanisa la Kiprotestant. Alimuoa mwanamke raia wa Poland na amefanikiwa kuzaa naye watoto wanne. Alichaguliwa kuwa mbunge na chama cha Civic Platform Party, baada kiti cha ubunge wa jimbo lake kuwa wazi baada ya aliyekuwa mbunge kukiacha kiti hicho alipochaguliwa kuwa meya. Kabla ya kuwa mbunge alikuwa mjumbe wa baraza la halmashauri ya mji wa Lodz. Kuhusiana na ubaguzi wa rangi nchini Poland, Godson alisema kuwa ubaguzi wa rangi nchini Poland umeanza kupungua katika miaka ya karibuni baada ya Poland kujiunga na Umoja wa Ulaya miaka sita iliyopita. Akiongea na radio moja ya nchini humo, Godson alisema: "Mimi natoka Lodz (jimbo analoliwakilisha, nitaishi hapa, nitafia hapa na nataka nizikwe hapa". | ||
Kituko! washitakiwa wavua nguo mahakamani
Kituko hicho kilitokea jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya jijini Dare s Salaam majira ya mchana.
Washitakiwa hao ambao ni Samuel Joseph, Saidi Idd na Said Zakaria walikuwa wakikabiliwa na mashitaka ya unyang’anyi wa kutumia silaha kesi ambayo ilikuwa ikiendeshwa mahakamani hapo yenye namba 184 ya mwaka 2010.
Hakimu Mkazi Ritha Tarimo aliwaachia huru washitakiwa hao majira ya saa 6 mchana kupitia kifungu namba 225[4] cha sheria ya mwenendo ya makosa ya jinai ya mwaka 1985 kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002 baada ya wakili wa serikali Leornad Chalo kudai upande wa mashitaka hawakuwa na jalada la polisi la kesi hiyo.
Hivyo hakimu huyo aliwaachia huru washitakiwa hao na punde tu hakimu aliamuru kukamatwa kwa washitakiwa hao na kurudishwa mahakamani kitendo ambacho washitakiwa hao hawakuafiki kwa muda huo kupinga kukamatwa tena huku akipiga kelele waachiwe.
Kufuatia hali hiyo askari polisi walitumia nguvu za ziada washitakwia hao kuwakamata na washitakiwa hao walichukua uamuzi wa kuvua nguo zao kupinga hukumu hiyo na hata askari polisi walipowataka wavae nguo waligoma na askari kuwafikisha mahakamani humo wakiwa hivyohivyo utupu kama walivyozaliwa.
Awali washitakiwa hao walifikishwa mahakamani kwa hati ya mashtaka iliyodai kuwa, mnamo Juni 4 mwaka huu, majira ya saa 9:00 jioni wakiwa maeneo ya Mchikichini jijini Dar es Salaam, waliiba vitu mbalimbali zikiwemo simu mbili za mkononi aina ya Samsung na Nokia pamoja na nyaraka mbalimbali vyote vikiwa na thamani ya Sh.467,000 mali ya David Mkombozi na kabla ya kufanya wizi huo walidaiwa kumjeruhi mwenye mali hizo kwa kumkatakata na panga kichwani li waweze kujinyakulia mali hizo.

Tibaijuka aamuru kuta zivunjwe
Agizo alilitoa jana akiwaamuru viongozi wa Manispaa ya Ilala kutekeleza agizo hilo mara moja wakati wa ziara yake alipotembelea maeneo ya wazi yaliyochukuliwa kiholela.
Waziri Tibaijuka akiwa na ujumbe wake wakiwemo watendaji wakuu wa wizara hiyo, wakuu wa wilaya walitumia usafiri wa daladala kutembelea maeneo hayo.
Akifuata ramani ya mipango miji walipofika kwenye kiwanja namba 59 kilichopo Ocean Road, waziri huyo aliamuru kuvunjwa kwa ukuta uliozungushiwa eneo hilo kwa kuwa ramani inaonyesha eneo hilo kuwa ni la wazi.
Mara bada ya ktuoa amuri hiyo Tibaijuka alitoa agizo kuwa mara bada ya kubomolewa kwa kuta hizo aliwaagiza kuwa maeneo hayo yatengenezwe bustani kwani maeneo hayo ni ya wananchi na si kama walivyojichuklia kiholewa kwa matumizi yao binafsi.
Eneo hilo lilidaiwa kuwa lilimilikishwa kwa Jumuiya Shree Hindu Mandal mwaka 1952 kwa matumizi ya kuchomea maiti.
Pia Tibaijuka aliamuru eneo la Palm Beach pavunjwe kwa kuwa Rais mstaafu wa wamu ya tatu Benjamin Mkapa alishatengua umiliki wa eneo hilo kutoka kwa wamiliki wawili waliojulikana kama Shantaben Patel na G. Patel kwa kuwa eneo hilo lilikuwa na mgogoro, pia kuvunjwa kwa nyumba iliyokuwan ndani ya ukuta huo.
Pia eneo la Msasani Bonde la Mpunga aliona limekaa shabagala na kuitaka serikali kufanya uwezekano wa kuwapa nyumba wakazi hao ili eneo hilo liweze kuwekwa katka mpangilio unaofaa.
Pia eneo la Bonde la Msimbazi alisema linahitaji marekebisho kujenga nyumba ili ziweze kusaidia wananchi.
Katika ziara hiyo pia alikuwemo mbunge wa jimbo la Ubungo, John Mnyika, Halima Mdee wa Kawe na kuitaka ziara hiyo kufika majimboni humo kwani kuna viwanja vya wazi vilivyomilikiwa na watu isivyo halali.

Jitokezeni kupima afya ya moyo bure
Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa Klabu ya Lions, Bw. Frank Goyayi, ambapo alifafanua kambi hiyo itaanza siku ya Ijumaa itafanyika katika hospitali ya Regency Upanga jijini Dar es Salaam.
Goyayi alisema kuwa, katika uchinguzi huo daktari bingwa wa maradhi ya moyo, Ashutosh Marwah, kutoka taasisi ya moyo ya Fortis Escorts, India atakayeendesha shughuli hiyo.
Alifafanua kuwa watoto watakaogundulika wana matatizo hayo watagawanywa ambapo 50 watatoka Bara nakutoka bara na 50 kutoka visiwani Zanzibar ambao watapelekwa India kwa matibabu.
Hivyo wakazi wajiji wametakwia kujitokeza kupima afya hiyo na watakaogundulika kupelekwa kwa matibabu India.
Taasisi hiyo imekwua ikijitahidi wka hali na mali kusaidia wnanchi wa vipato vya chini kuwasidia kuwatibu maradhi hayo

Sala ya Myahudi Yasababisha Kizaazaa Kwenye Meli
Tukio hilo lilitokea jana jumapili katika mji wa Picton nchini New Zealand wakati mtalii huyo wa Israel alipotoa viboksi viwili vyeusi na kujifunga mkononi na usoni kabla ya kuanza kusali kwa sauti katika lugha ambayo hakuna mtu katika meli hiyo aliyeielewa. Polisi wa kikosi maalumu cha kupambana na ugaidi wakiwa na silaha waliivamia meli hiyo na kumweka chini ya ulinzi mtalii huyo wa Israel kabla ya kumshusha toka kwenye meli hiyo pamoja na jamaa zake alioambatana nao kwa mahojiano zaidi. Kwa mujibu wa gazeti la Dominion Post, wafanyakazi wa meli hiyo iliyokuwa imebeba abiria 750 walishtuka kumuona mtalii huyo wa Israel akitoa viboksi viwili vyeusi toka kwenye begi lake na kujifunga mkononi na kwenye paji lake la uso. Wafanyakazi hao walitoa taarifa polisi ambapo kikosi maalumu kikiwa na silaha nzito kilivamia meli hiyo na kumweka chini ya ulinzi mtalii huyo. Akiliongea suala la mtalii huyo wa Israel kuwekwa chini ya ulinzi wakati akisali, afisa mmoja wa serikali ya New Zealand alisema kuwa tukio hilo limetokea kwa bahati mbaya kutokana na hofu kubwa ya ugaidi iliyopo nchini humo. | ||
GURUMO APATA NAFUU, DK. REMMY...
Yule mwanamuziki mkongwe hapa nchini aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Bendi ya Muziki wa Dansi ya Msondo Ngoma, Muhidini Maalim Gurumo hatimaye amepata ahueni na anatarajiwa kuruhusiwa kurudi nyumbani muda wowote kuanzia sasa.
Jinsi ya kujisafisha na dhambi ya usaliti
Zifuatazo ni njia sahihi zinazoweza kusaidia kumsafisha mtu aliyenaswa kwenye usaliti.
KWANZA: Ikiwa utajikuta upo kwenye dhambi ya usaliti ambayo huwezi kuikana njia ya kwanza kufanya ni kukiri kosa mbele ya mwenza wako na kumweleza mazingira yaliyosababisha wewe kufikia hatua ya kufanya usaliti.
“Nakiri mke wangu kuwa nimekosa kilichotokea kwenye hili ni kwamba huyu mwanamke nilikuwa naye tangu zamani na huwa haishi hapo lakini wiki hii alikuja jijini akanipigia simu nikakutana naye ndiyo hapo ibilisi alipoanza, lakini kusema kweli najuta kukukosea.” Huu ni mfano wa maneno ya kukiri kosa kwa kueleza sababu za usaliti wako.
PILI :Naamini kuna watu ambao hufanya usaliti kwa sababu ya dhaifu, hawa ni wale ambao tabia zao si za kujali heshima ya ndoa zao. Kwa hawa na wengine lazima hatua ya pili iwe ni kubadili mfumo wa maisha yao kwa ujumla.
Kwa mfano, ikiwa mtu amegundulika kuwa hufanya usaliti anapochelewa sana kurudi nyumbani au anapokuwa kwenye kumbi za starehe usiku, anachotakiwa kufanya ni kubadili mfumo mzima wa maisha yake ikiwa ni pamoja na kuacha kuchelewa na kwenda kwenye kumbi za usiku hapa ndipo atakapokuwa na nafasi ya kusamehewa na kuaminiwa.
TATU: Toba ya kweli yenye kuaminika lazima iambatane na matendo. Unapojikuta kwenye dhambi ya kusaliti lazima utubu kwa matendo yatakayoonyesha kweli unampenda mpenzi wako zaidi ya yule uliyekuwa naye. Hapa mambo ya zawadi, huduma na kujali lazima yachukue nafasi kubwa, lengo ni lile lile kujenga imani zaidi.
NNE: Kama kweli utakuwa umedhamiria kuomba radhi, basi lazima muonekano wako na maneno yako yatafsiri nia yako. Haiwezekani ukawa unamuomba radhi mtu huku ukitembea tembea na kuonyesha mzaha na hali ya uchangamfu kana kwamba ulichokifanya kilikuwa sahihi.

BREAKING NYUUUUZZZZ: KILIMANJARO STARS MABINGWA WAPYA WA CECAFA
TAIFA STARS IMETWAA UBINGWA WA KOMBE LA TUSKER CECAFA CHALLANGE CUP BAADA YA KUIDUNGUA IVORY COAST 1-0 KATIKA MCHEZO WA FAINALI WA MICHUANO HIYO ILIYOMALIZIKA SASA HIVI NESHNO JIPYA JIJINI DAR.
MFUNGAJI WA BAO HILO NI NAHODHA SHADRACK NSAJIGWA KWA NJIA YA PENATI BAADA YA BEKI WA IVORY COAST KUUNAWA MPIRA KWENYE DAKIKA YA 31.
UWANJA UMELIPUKA KWA NDEREMO NA VIFIJO HIVI SASA NA WAKATI WOTE WAZIRI WILLIAM LUKUVI AMBAYE NI MGENI RASMI ATAKABIDHI KOMBE NA ZAWADI KWA WASHINDI.
Transfoma ya Chalinze yahamishiwa Dar kupunguza makali ya mgao
Tayari wizara hiyo imeshaagiza wakandarasi wa shirika la umeme kuhamisha transfoma hiyo ije jijini Dar es Salaam ifungwe katika kituo cha Kipawa na iwashwe kwa madhumuni ya kupunguza makali ya mgao wa umeme.
Wizara hiyo imetoa siku nane shughuli za ufungaji transofoma hiyo umalizike.
Transfoma hiyo imechukuliwa kutoka Chalinze ilikuwa ni ya mradi mwingine wa kuboresha umeme katika mikoa ya Pwani,Tanga, Mwanza na Shinyanga.
Bw. Abdulah Feresh, Meneja Mwandamizi wa Udhibiti Mifumo na Njia Kuu za Umeme alisema kwa muda huo uliotolewa wataweza kumaliza kazi hiyo kwa kuwa watahakikisha wanafanya kazi kwa saa 24 kila siku.

Baba Amzalisha Binti Yake Watoto 10
Tukio hili la Argentina linakumbushia kesi ya Josef Fritzl wa Austria ambaye alihukumiwa kwenda jela maisha baada ya kumfungia kwenye kichumba binti yake na kumbaka na kumzalisha jumla ya watoto 7.
Katika kesi ya Argentina, mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 62 ambaye jina lake liliwekwa kapuni, alikanusha kumbaka binti yake lakini vipimo vya DNA vilithibitisha kuwa watoto wote 10 aliowazaa binti yake ni wa kwake.
"Mtuhumiwa alikanusha kumbaka binti yake lakini vipimo vya DNA vimethibitisha kuwa ni watoto wake", alisema jaji Virgilio Palud alipokuwa akiongea na mojawapo ya radio za Argentina.
Mtuhumiwa huyo alimbaka binti yake mara nyingi sana kwa muda wa miaka 30 kosa ambalo adhabu yake ni kwenda jela miaka 20, alisema jaji Palud.
Binti wa mtuhumiwa ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 43, alisema kuwa baba yake alianza kumbaka tangu alipokuwa na umri wa miaka 13.
Binti huyo wa mtuhumiwa alisema kuwa alisubiri muda mrefu kumtia hatiani baba yake kwakuwa baba yake alikuwa akitishia kumuua iwapo atatoa siri nje. Aliamua kuripoti siri hiyo polisi baada ya baba yake kukamatwa na polisi kwa kuiba mifugo.
"Hii ni kesi mbaya kuliko hata ya Josef Fritzl wa Austria", alisema jaji Palud.
Hii ni kesi ya pili kutokea nchini Argentina ambapo baba wakware waliwabaka watoto wao.
Mwaka jana, kesi ya baba wa nchini Argentina aliyembaka na kumzalisha binti yake watoto saba, ilichukua nafasi kubwa sana kwenye vyombo vya habari nchini Argentina.

Obama Achanika Mdomo Baada ya Kupigwa 'Kipepsi'

Msemaji wa ikulu ya Marekani alisema kuwa Obama alipasuka mdomo na alipatiwa matibabu na madaktari wa ikulu.
Hata hivyo taarifa ya ikulu ya Marekani haikusema ni nani ndiye aliyempasua Obama mdomo wake kwa kiwiko.
Nyota wa Sinema Amuua Mama Yake Akidai ni Shetani
Michael Brea mwenye umri wa miaka 31, nyota wa filamu ya "Step Up 3D" na tamthilia maarufu ya "Ugly Betty" ametupwa rumande akisubiria hukumu yake kwa kumuua mama yake kwa jambia. "Sikumuua yeye, nimemuua shetani aliyekuwa ndani ya mwili wake", alisema Brea alipokuwa akiongea na gazeti la New York Daily News akiwa kwenye wadi ya hospitali ya jela ambako aliwekwa tangu alipotiwa mbaroni kwa kosa la mauaji. "Niliendelea kumkatakata vipande vipande na hakuna mtu aliyeweza kunizuia. Nilikuwa nikifanya kazi ya mungu", aliendelea kusema Brea. Kwenye majira ya saa saba na nusu usiku siku ya jumanne majirani walisikia kelele Brea akimwambia mama yake "Tubia tubia" huku akimsomea mistari ya biblia. Majirani walisema kuwa Brea alikuwa akimkimbiza mama yake nyumba nzima huku akimlazimisha atubie. Majirani waliita polisi ambao walipofika walikuta tayari Brea ameishamchinja mama yake. Maiti ya mama yake, Yanick Brea, 55, ilikutwa bafuni ndani ya nyumba yake iliyopo Brooklyn, taarifa ya polisi ilisema. Brea, alikutwa na polisi akiwa amekaa chumbani huku ameshikilia jambia lenye urefu wa futi tatu. Ndugu wa marehemu wametoa taarifa ya kuonyesha kumtetea Brea ambaye wamesema alikuwa ni mwanaume mpole, mwenye huruma na mwenye mapenzi kwa mama yake lakini alikuwa akihitaji msaada kwa matatizo yaliyokuwa yakimkabili. "Familia yake na marafiki zake wanajua fika kuwa Michael hakuwa akijitambua wakati alipokuwa akimuua mama yake", ilisema taarifa ya familia ya Brea. | ||
Chupi za Mitumba Marufuku Ghana
Wapenzi wa viwalo vya ndani vilivyotumika majuu nchini Ghana wana miezi michache ya kununua viwalo vyao baada ya nguo hizo za mitumba kupigwa marufuku nchini humo. Bodi ya viwango ya Ghana imetangaza kuwa kuanzia mwezi februari mwakani, itakuwa ni kinyume cha sheria kuuza chupi na sidiria zilizotumika ambazo huingizwa nchini humo kama mitumba kutoka nchi za ulaya. Ghana ilipitisha sheria ya kupiga marufuku mitumba ya nguo za ndani mwaka 1994 lakini ilishindwa kusimamia utekelezaji wa sheria hiyo. Lakini hivi sasa bodi ya viwango ya Ghana imetangaza kuwa itasimamia kikamilifu utekelezaji wa sheria hiyo kuanzia mwezi februari mwakani. Wafanyabiashara wa mitumba wamelalamika kuwa ajira zao zitapotea sheria hiyo itakapoanza kutekelezwa mwakani. Serikali ya Ghana imesema kuwa sheria hiyo ni kwaajili ya kulinda afya za wananchi wake. | ||
Kivumbi Ivory Coast, Wagombea Wajiapisha Wenyewe Kuwa Marais
Hali si shwari nchini Ivory Coast kufuatia vurugu na vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyokaribia kutokea nchini humo baada ya wagombea urais kuamua kujiapisha wenyewe kuwa marais.
Kizaa zaa kilianza baada ya tume ya uchaguzi kumtangaza mgombea wa kambi ya upinzani, Alassane Ouattara ameshinda uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika novemba 28.
Lakini mahakama ya katiba iliyafuta matokeo ya uchaguzi katika sehemu za kaskazini mwa nchi hiyo na kumtangaza Rais aliyemaliza muda wake, Laurent Gbagbo ndiye mshindi.
Wakati hali ikiwa tete, Gbagbo alijiapisha mwenyewe kuwa rais na ndipo Ouattara alipoamua na yeye kujipisha kuwa rais.
Umoja wa mataifa, Umoja wa ulaya na umoja wa mataifa ya Afrika unayakubali matokeo ya mgombea wa upinzani kushinda uchaguzi huo.
Rais wa Marekani, Barack Obama, Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy wote walimpongeza Alassane Ouattara kwa kushinda uchaguzi huo na kuntaka rais aliyemaliza muda wake akubali matokeo ya kushindwa kwenye uchaguzi huo.
Rais Laurent Gbagbo anatetewa na jeshi la nchi hiyo wakati Alassane Ouattara analindwa na kupewa tafu na majeshi ya umoja wa mataifa.
Hali imekuwa mbaya zaidi kufuatia vurugu zinazoendelea nchini humo ambazo zimepelekea vifo vya watu 17 hadi sasa.
Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki ameenda nchini Ivory Coast kujaribu kusuluhisha mgogoro huo.

ANASWA GESTI NA DENTI WA MIAKA 10
Mfanyabiashara huyo ambaye aligoma kutaja jina lake, alinaswa akiwa na denti wa miaka 10, wakiingia Gesti ya Green, Sinza, Dar es Salaam.
Habari zinasema kuwa mhudumu wa gesti hiyo (jina tunaliminya) alikuwa wa kwanza kumtilia shaka mfanyabiashara huyo kabla ya wananchi wenye hasira kuingilia kati na kumpa kipigo chenye uzani mkubwa.
Siku hiyo, majira ya saa nane alasiri, denti huyo (jina lake na la shule kapuni), akiwa na sare za Shule eneo la Legho, Sinza, alisimamishwa na mfanyabiashara huyo aliyekuwa ndani ya taksi.
JK asamehe wafungwa, mafataki, mafisadi awabakisha gerezani
RAIS Jakaya Kikwete jana alitoa msamaha kwa wafungwa wapatao 3563, waliotumika kifungo kwa muda mrefu gerezani na kuwaacha wale wabakaji na waliowaharibia wanafunzi masomo yao maarufu kama [mafataki]
Ili Kumuua Mchawi Wachoma Moto Kituo cha Polisi
Kamanda wa polisi mkoani Rukwa, Isuto Mantage, alisema wanaoshikiliwa na polisi ni wakazi wa kijiji cha Wampembe wilaya ya Nkasi baada ya jaribio lao kukitekeza kwa moto ili kumuua mzee Daud Kapelo (76) waliyemtuhumu kwa uchawi. Alisema, chanzo cha tuhuma hizo ni kifo cha Joseph Kapelo (19) aliyeugua kwa muda mfupi na kufa Novemba 22 mwaka huu na kuibua imani za kishirikina wakimhusisha baba wa marehemu, Kapelo (76), na kifo hicho. Alisema, wakati wananchi hao wakipanga mikakati hiyo, taarifa zilifika kituo kidogo cha polisi cha Wampembe na kufanikisha polisi kumwokoa mtuhumiwa huyo aliyekuwa amejeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake na wananchi wenye hasira. Kamanda huyo alieleza kwamba wakati wananchi hao wakielekea makaburini, walilipeleka jeneza la marehemu hadi kituo cha polisi na kuliweka wakimtaka Daud atolewe mahabusu ili naye wammalize kisha kumzika pamoja na mwanaye. “Vurugu za wananchi wale ziliendelea na kuanza kushambulia kituo cha polisi kwa mawe hali iliyowalazimu askari waliokuwepo zamu kupiga risasi hewani lakini wananchi hao hawakuogopa na kuanza kumshambulia askari huyo na kuibua mapigano kati ya askari na wananchi,” alisema. Alisema, wananchi hao waliwasha moto uliozimwa kwa msaada wa askari na mgambo waliokuwepo kabla ya wananchi hao kutawanyika. Kamanda huyo alibainisha kwamba wakati wa mapambano hayo, Imelda Kayanda (46), alipigwa risasi na kufariki huku naye Agnes Kisori (21) akijeruhiwa mguuni ambapo walikimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi. Kadhalika, jeshi hilo limewatia mbaroni Zakaria Francis (28), Ikombe Yustini (39), Stephano Kambe (18), Benard Kabeja (16), John Kapandila (22), Said Diwali (36), Vido Tuwakazi (21), Abdalah Vicent (19), Sylveter Kapala (17), Richad Bushota (19), John Mathias (58), Wilbroad Chambi (16) na Kapondo Anatoli (23). Kamanda huyo alisema, watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika na polisi wataendelea kuwatafuta waliokimbia. Aidha Kamanda Mantage, alitoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mikononi na kuvamia vituo vya polisi. |
Kumbi za starehe Bongo kufungiwa
Upo uwezekano mkubwa wa kumbi nyingi za starehe Bongo kufungiwa kutokana na tamko lililotolewa na serikali hivi karibuni kuwa, kumbi zote ambazo hazijasajiliwa hazitakiwi kuendelea kufanya kazi.
Akizungumza katika kikao kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Ghonche Materego alisema kuwa, zoezi zima la kuzihakiki kumbi hizo litafanywa na Kampuni ya Majembe ambao wamesaini nao mkataba.
“Tumeingia mkataba wa mwaka mmoja na Kampuni ya Majembe kuhakikisha kumbi zote za starehe zinasajiliwa, zile zitakazobainika kuendeshwa kiujanjaujanja hatua za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pomoja na kuzifungia,” alisema Materego.
Kufuatia mpango huo, imetabiriwa na baadhi ya wadau wa burudani nchini kuwa, kuna uwezekano kumbi nyingi zikafungiwa kufuatia uwepo wa nyingi ambazo hazijasajiliwa.

Efrancyia Mangii mshiriki wa Kinyang’anyiro cha Maisha Plus Season I 2007/08,
Baada ya kudaiwa kukwapua simu ya jamaa aliyetajwa kwa jina la Brockway Mchana ‘Karume’, mshiriki wa Kinyang’anyiro cha Maisha Plus Season I 2007/08, Efrancyia Mangii ametoboa kuwa, mapenzi ndiyo yaliyombebesha skendo hiyo nzito ya wizi.
Subscribe to:
Posts (Atom)