Washitakiwa hao walifikishwa katika mahakama ya mkoa wa Arusha na kusomea mashitaka.
Waliopandishwa kizimbani ni Mwenyekiti wa Chama hicho pia ni Mbunge wa Hai mkoani Kilimanjaro Freeman Mbowe{49}, Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilbrod Slaa {62}, Mbunge wa jimbo la Moshi mjini, Philimon Ndesamburo {77},Godblles Lema Mbunge wa Arusha mjini{34} na Joseph Selasin{50} mbunge wa jimbo la Rombo mkoani Kilimanjaro.
Walisomewa mashitaka mbele ya hakimu mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo,Charles Magesa na upande wa mashitaka ulikuwa ukiendeshwa na Mwendesha mashtaka wa serikali, Haruni Mategara na Zacharia Isalia.
Ilidaiwa kuwa washitakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa hilo Januari 5 mwaka huu, majira ya mchana kwa kufanya na kusababisha mkusanyiko na maandamano yaliyopigwa marufuku na jeshi la polisi huko mkoani Arusha.
Washitakiwa wote waliachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni mbili kila mmoja, na kesi hiyo itatajwa tena januari 21 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment