Matatizo ya kiufundi zakwamisha noti mpya

Noti hizo zilitarajiwa kuingia katika mzunguko wa fedha Januari Mosi na zimekwama kutokana na sababu iliyoelezwa kutoka ndani ya benki hiyo.

Noti hizo tarajio zinatarajiwa kuwa katika sura mpya kw kuweka alama mpya za “GEMINI and SPARK” ndani ya noti hizo na kuwa katika ubora stahili utakakidhi haja za watanzania zikiwa na uwezo wa kudumu kwa muda mrefu kuliko awali.

Pia noti hizo za shilingi 500 na 1,000 zitakuwa na waasisi wa Taifa akiwemo Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, na hayati Abeid Amani Karume wa Zanzibar.

Na katika noti za Sh. 2,000, 5,000 na 10,000 zimeendelea kuwa na picha za maliasili za misitu na wanyama wa taifa, na kutakuwa na mabadiliko ya ukubwa katika noti hizo.

Viongozi Chadema Mbaroni wapewa dhamana ya Mil .2 kila mmoja

Washitakiwa hao walifikishwa katika mahakama ya mkoa wa Arusha na kusomea mashitaka.

Waliopandishwa kizimbani ni Mwenyekiti wa Chama hicho pia ni Mbunge wa Hai mkoani Kilimanjaro Freeman Mbowe{49}, Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilbrod Slaa {62}, Mbunge wa jimbo la Moshi mjini, Philimon Ndesamburo {77},Godblles Lema Mbunge wa Arusha mjini{34} na Joseph Selasin{50} mbunge wa jimbo la Rombo mkoani Kilimanjaro.


Walisomewa mashitaka mbele ya hakimu mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo,Charles Magesa na upande wa mashitaka ulikuwa ukiendeshwa na Mwendesha mashtaka wa serikali, Haruni Mategara na Zacharia Isalia.

Ilidaiwa kuwa washitakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa hilo Januari 5 mwaka huu, majira ya mchana kwa kufanya na kusababisha mkusanyiko na maandamano yaliyopigwa marufuku na jeshi la polisi huko mkoani Arusha.

Washitakiwa wote waliachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni mbili kila mmoja, na kesi hiyo itatajwa tena januari 21 mwaka huu.

NI SOOOOOOO!

Mkuu wa Wilaya Acharazwa Bakora

Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 23 wa nchini Peru ambaye alichaguliwa kuwa mkuu wa wilaya alitumia njia ya aina yake ya kujikumbusha ahadi alizozitoa wakati wa kampeni wa uchaguzi.

Abraham Carrasco baada ya kuchaguliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Chilca, aliamua kuwaita watu kushuhudia akicharazwa bakora kabla ya kula kiapo cha kuitumikia wilaya hiyo.

Mbele ya mamia ya watu waliokusanyika, mkuu huyo wa wilaya alicharazwa bakora tatu ili azikumbuke ahadi alizozitoa wakati wa uchaguzi.

Carrasco alimchagua mzee mmoja aliyekuwa akiheshimika katika wilaya hiyo ndio amcharaze bakora kabla ya kula kiapo.

"Usiwe mwizi", alicharazwa bakora ya kwanza, "Usiwe muongo", alicharazwa bakora ya pili "Usiwe mvivu", alicharazwa bakora ya tatu.

Baada ya kucharazwa bakora, Carrasco alimbusu mikono mzee aliyemchapa bakora na kisha kula kiapo cha kuitumikia vyema na kwa uadilifu wilaya hiyo.

Carrasco alisema kuwa ataihifadhi bakora iliyotumika ili iwe kumbukumbu yake kwa ahadi alizozitoa wakati wa kampeni za uchaguzi.