Noti hizo zilitarajiwa kuingia katika mzunguko wa fedha Januari Mosi na zimekwama kutokana na sababu iliyoelezwa kutoka ndani ya benki hiyo.
Noti hizo tarajio zinatarajiwa kuwa katika sura mpya kw kuweka alama mpya za “GEMINI and SPARK” ndani ya noti hizo na kuwa katika ubora stahili utakakidhi haja za watanzania zikiwa na uwezo wa kudumu kwa muda mrefu kuliko awali.
Pia noti hizo za shilingi 500 na 1,000 zitakuwa na waasisi wa Taifa akiwemo Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, na hayati Abeid Amani Karume wa Zanzibar.
Na katika noti za Sh. 2,000, 5,000 na 10,000 zimeendelea kuwa na picha za maliasili za misitu na wanyama wa taifa, na kutakuwa na mabadiliko ya ukubwa katika noti hizo.
edra123
Viongozi Chadema Mbaroni wapewa dhamana ya Mil .2 kila mmoja
Washitakiwa hao walifikishwa katika mahakama ya mkoa wa Arusha na kusomea mashitaka.
Waliopandishwa kizimbani ni Mwenyekiti wa Chama hicho pia ni Mbunge wa Hai mkoani Kilimanjaro Freeman Mbowe{49}, Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilbrod Slaa {62}, Mbunge wa jimbo la Moshi mjini, Philimon Ndesamburo {77},Godblles Lema Mbunge wa Arusha mjini{34} na Joseph Selasin{50} mbunge wa jimbo la Rombo mkoani Kilimanjaro.
Walisomewa mashitaka mbele ya hakimu mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo,Charles Magesa na upande wa mashitaka ulikuwa ukiendeshwa na Mwendesha mashtaka wa serikali, Haruni Mategara na Zacharia Isalia.
Ilidaiwa kuwa washitakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa hilo Januari 5 mwaka huu, majira ya mchana kwa kufanya na kusababisha mkusanyiko na maandamano yaliyopigwa marufuku na jeshi la polisi huko mkoani Arusha.
Washitakiwa wote waliachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni mbili kila mmoja, na kesi hiyo itatajwa tena januari 21 mwaka huu.
Waliopandishwa kizimbani ni Mwenyekiti wa Chama hicho pia ni Mbunge wa Hai mkoani Kilimanjaro Freeman Mbowe{49}, Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilbrod Slaa {62}, Mbunge wa jimbo la Moshi mjini, Philimon Ndesamburo {77},Godblles Lema Mbunge wa Arusha mjini{34} na Joseph Selasin{50} mbunge wa jimbo la Rombo mkoani Kilimanjaro.
Walisomewa mashitaka mbele ya hakimu mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo,Charles Magesa na upande wa mashitaka ulikuwa ukiendeshwa na Mwendesha mashtaka wa serikali, Haruni Mategara na Zacharia Isalia.
Ilidaiwa kuwa washitakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa hilo Januari 5 mwaka huu, majira ya mchana kwa kufanya na kusababisha mkusanyiko na maandamano yaliyopigwa marufuku na jeshi la polisi huko mkoani Arusha.
Washitakiwa wote waliachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni mbili kila mmoja, na kesi hiyo itatajwa tena januari 21 mwaka huu.
Mkuu wa Wilaya Acharazwa Bakora
Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 23 wa nchini Peru ambaye alichaguliwa kuwa mkuu wa wilaya alitumia njia ya aina yake ya kujikumbusha ahadi alizozitoa wakati wa kampeni wa uchaguzi. Abraham Carrasco baada ya kuchaguliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Chilca, aliamua kuwaita watu kushuhudia akicharazwa bakora kabla ya kula kiapo cha kuitumikia wilaya hiyo. Mbele ya mamia ya watu waliokusanyika, mkuu huyo wa wilaya alicharazwa bakora tatu ili azikumbuke ahadi alizozitoa wakati wa uchaguzi. Carrasco alimchagua mzee mmoja aliyekuwa akiheshimika katika wilaya hiyo ndio amcharaze bakora kabla ya kula kiapo. "Usiwe mwizi", alicharazwa bakora ya kwanza, "Usiwe muongo", alicharazwa bakora ya pili "Usiwe mvivu", alicharazwa bakora ya tatu. Baada ya kucharazwa bakora, Carrasco alimbusu mikono mzee aliyemchapa bakora na kisha kula kiapo cha kuitumikia vyema na kwa uadilifu wilaya hiyo. Carrasco alisema kuwa ataihifadhi bakora iliyotumika ili iwe kumbukumbu yake kwa ahadi alizozitoa wakati wa kampeni za uchaguzi. | ||
Siri za Marekani Zaanikwa Hadharani
Nyaraka za siri za Marekani zipatazo 250,000 zimeanza kuwekwa hadharani pamoja na serikali ya Marekani kuionya tovuti ya WikiLeaks kuwa inavunja sheria na inayaweka maisha ya watu wengi hatarini. Tovuti ya WikiLeaks ambayo imebobea kwa kutoboa siri za ndani za masuala mbalimbali duniani ilikabiliwa na mashambulizi ya hackers ambao waliifanya tovuti hiyo ishindwe kupatikana online. Hata hivyo nyaraka hizo za siri zimewekwa hadharani kama ilivyopangwa kwa kutumia magazeti ya The Guardian la Uingereza, gazeti la New York Times la Marekani, Der Spiegel la Ujerumani, El Pais la Hispania na gazeti la Le Monde la Ufaransa. Nyaraka hizo za siri huenda zikaharibu uhusiano wa Marekani na baadhi ya viongozi wa nchi mbalimbali duniani ambao Marekani iliwapachika majina mbalimbali ya kuwakashifu. Miongoni mwa nyaraka hizo za siri hizo ni mazungumzo ya siri kati ya Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia ambaye mara nyingi sana alikuwa akiishinikiza Marekani ipigane vita na Iran ili kuziteketeza silaha zake za nyuklia. Taarifa hizo ziliendelea kusema kuwa Mfalme huyo wa Saudia aliishinikiza Marekani iiwekee Iran vikwazo vikali vya kiuchumi na kuwapiga marufuku viongozi wake kusafiri kimataifa. Nyaraka hizo ziliendelea kusema kuwa Mfalme Abdullah aliungwa mkono na Mfalme wa Bahrain, Hamad ibn Isa Al Khalifa na Mtawala wa Abu Dhabi, Sheikh Mohammad bin Zayed ambao nao waliitaka Marekani iiteketeze Iran. WikiLeaks pia ilitoa nyaraka ambazo zilisema kuwa Marekani kwa kuwatumia maafisa wake kinyume cha sheria iliwapeleleza viongozi wa baraza la Umoja wa Mataifa na hata kufikia kuchukua kwa siri alama za mboni ya jicho na alama za vidole za katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon. Marekani pia ilifuatilia simu walizokuwa wakipiga, fax, email na tovuti walizokuwa wakizitembelea. Miongoni mwa majina ya kashfa waliyopachikwa viongozi wa serikali mbalimbali duniani, Marekani ilimuita Rais Mugabe wa Zimbabwe kuwa ni "Kichaa Mzee", kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi ameitwa "Mtu wa Ajabu Asiyeeleweka", wakati rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad amefananishwa na Hitler. Nyaraka nyinginezo zilielezea jinsi Marekani ilivyokuwa ikizishinikiza baadhi ya nchi ziwachukue wafungwa wa kigaidi wa jela ya Guantanamo Bay. Nchi ya Slovenia ililazimishwa imchukue mfungwa mmoja wa Guantanamo Bay iwapo inataka kukutana na Rais Obama. Nyaraka zaidi za siri zinazoonyesha jinsi Marekani ilivyokuwa ikivunja sheria za kimataifa zinaendelea kuchapishwa. | ||
Kitabu cha Mafunzo ya Wizi
Mwizi wa nchini Japan, Hajime Karasuyama kutokana na utaalamu wake wa kuiba kwenye majumba ya watu, ametoa kitabu kinachoelezea jinsi ya kuiba kwa ustadi mkubwa bila ya kugundulika. Kitabu chake kinachoenda kwa jina la "Kazi: Mwizi, Kipato Kwa mwaka: Yen Milioni 30", kimekuwa gumzo nchini Japan na kimekuwa kikinunuliwa kama njugu. Wachapishaji wa kitabu hicho Futabasha Publishing wamesema kuwa nakala za mwanzo za kitabu hicho zipatazo 10,000 zimenunuliwa zote ndani ya siku 10 baada ya kitabu hicho kuzinduliwa. Katika kitabu hicho, Karasuyama anaelezea jinsi ya kufungua vitasa vya milango ya aina yoyote ile kwa muda mfupi na bila ya ufunguo na jinsi ya kuvunja madirisha ya vioo bila ya kusababisha kelele. Karasuyama ameelezea pia jinsi alivyokuwa akitumia lensi kuangalia ndani ya nyumba kwa kupitia kwenye tundu la funguo. Mbali ya wizi wa majumbani, Karasuyama pia amelezea pia njia za kufanya utapeli na kuwaacha watu kwenye mataa. Karasuyama alisema kuwa kutokana na wizi alikuwa akijiingizia kitita kinono kwa mwaka zaidi ya Tsh. Milioni 540. "Tunapoingia ndani ya nyumba, sisi wezi huwa tunajua wapi watu huficha pesa zao", alisema Karasuyama alipokuwa akiongea na jarida la Shukan Taishu kuhusiana na kitabu chake ambacho kimeambatanisha maneno ya "Usijaribu kuniiga" kwenye ukurasa wake wa kwanza. Wachapishaji wa kitabu hicho kinachouzwa Yen 1,200 sawa na Tsh. 20,000 wamekanusha madai kuwa kuchapishwa kwa kitabu hicho kutapelekea baadhi ya watu kugeuka wezi kwa kuiga staili za wizi za Karasuyama. Wachapishaji hao wamesema kuwa kitabu cha Karasuyama kitawawezesha watu kujifunza njia zinazotumiwa na wezi hivyo kuweza kuzilinda vyema nyumba zao. | ||
Mnigeria Awa Mbunge Wa Kwanza Mweusi Nchini Poland
John Abraham Godson, alizaliwa katika jimbo la Abia nchini Nigeria na alikulia nchini humo kabla ya kuhamia nchini Poland. Godsnon ambaye ni msomi mwenye shahada nyingi, amekuwa gumzo nchini Poland baada ya kuingia kwenye vitabu vya historia ya masuala ya siasa nchini humo kwakuwa mtu mweusi wa kwanza kuwa mtunga sheria wa bunge la nchi hiyo ambayo bado ina matatizo ya ubaguzi wa rangi. Godson alishawahi kuonja joto la ubaguzi wa rangi nchini humo kwa kushushiwa kipigo mara mbili bila ya sababu za msingi. Godson alihamia Poland mwanzoni mwa miaka ya 1990 na kuanzisha shule ya Kiingereza na pia kufanya kazi kama mchungaji wa kanisa la Kiprotestant. Alimuoa mwanamke raia wa Poland na amefanikiwa kuzaa naye watoto wanne. Alichaguliwa kuwa mbunge na chama cha Civic Platform Party, baada kiti cha ubunge wa jimbo lake kuwa wazi baada ya aliyekuwa mbunge kukiacha kiti hicho alipochaguliwa kuwa meya. Kabla ya kuwa mbunge alikuwa mjumbe wa baraza la halmashauri ya mji wa Lodz. Kuhusiana na ubaguzi wa rangi nchini Poland, Godson alisema kuwa ubaguzi wa rangi nchini Poland umeanza kupungua katika miaka ya karibuni baada ya Poland kujiunga na Umoja wa Ulaya miaka sita iliyopita. Akiongea na radio moja ya nchini humo, Godson alisema: "Mimi natoka Lodz (jimbo analoliwakilisha, nitaishi hapa, nitafia hapa na nataka nizikwe hapa". | ||
Subscribe to:
Posts (Atom)